FEZA KESSY KUWASILI NCHINI LEO
Mshiriki
wa Tanzania aliyetolewa kwenye shindano la Big Brother 'The Chase' Feza
Kessy, atawasili nchini leo (Jumatano) jioni saa kumi na mbili na
nusu kwa ndege ya South African Airways. Feza aliondolewa katika
shindano la la Big Brother 'The Chase'
Jumapili iliyopita na kuungana na Mtanzania mwenzake Ammy Nando
aliyetangulia kutoka katika jumba hilo. Wadau mnaombwa kujitokeza
kumpokea mshiriki wetu hapo kesho.