LICHA
ya kuonekana sharobaro, msanii mwenye makeke mengi awapo stejini, Ali
Salehe Kiba juzikati alinaswa na kamera zetu akipika vitumbua huku
akionekana mwenye uzoefu katika mapishi hayo.
Mpango
mzima ulikuwa nyumbani kwao maeneo ya Kariakoo jijini Dar ambapo jamaa
huyo alibambwa akiwa katika mishemishe za kuandaa vitafunio hivyo
ambavyo vilikuwa sehemu ya futari waliyoiandaa yeye na familia yake kwa
ajili ya kuwafuturisha watu.
Kitendo hicho kiliwafurahisha mashabiki wake ambapo baadhi yao
walisikika wakisema kuwa, msanii huyo ni mfano wa kuigwa kwani ni staa
mkubwa sana lakini anapenda kujichanganya na kutosahau asili yake.