AFYA YA MSANII MATUMANI IMEIMARIKA KIDOGO NA AMEREJEA TENA KATIKA FANI YAKE YA UIGIZAJI
BAADA ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo,
Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza
kujikongoja katika kazi ya uigizaji.Akiongea na mwandishi wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa
anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali
anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake
mwenyewe.
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa
nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema
Matumaini.
Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo
kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili
yake jambo ambalo siyo la kweli.