

“Baada ya kumlipa dalali, niliwatuma watu wakafanye usafi lakini wakashangaa kumkuta Wolper anahamishia vyombo vyake kwenye nyumba hiyo.
“Waliponipa taarifa nilichanganyikiwa sana kwani nilishalipa shilingi milioni tatu na laki sita ikiwa ni kodi ya miezi sita hivyo niliamua kukimbilia kwenye Kituo ha Polisi cha Magomeni kufungua kesi ili nisaidiwe kuipata nyumba hiyo au nirudishiwe fedha zangu,” alisema Baby Madaha.
“Hata hivyo, rafiki yangu Mariam Mndeme alijaribu kuongea na Wolper ili atupe ushirikiano wa kupata haki yangu lakini hakutaka kutusaidia,” alisema Baby.
Gazeti hili lilimtafuta Wolper na kumuuliza kuhusu ishu hiyo ambapo hakupenda kuongea mengi bali alimuunganisha mwandishi wetu na mwenye nyumba, Zulfa ambaye alisema kuwa mpangaji wake aliyeandikishana naye mkataba ni Wolper na kama kweli Baby alilipa fedha kwa dalali, basi ametapeliwa.
“Jamani hii ishu hainihusu kabisa, ukweli ni kwamba hao akina Baby wametapeliwa, umemsikia mwenye nyumba alichokisema kwa hiyo sitaki mnihusishe kabisa kuhusishwa na mambo hayo,” alisema Wolper.