UKURASA WA HABARI ZA MICHEZO MIKATAIFA: Mancini anasema Kurejea kwa Mourinho Premier League kutachangamsha ligi' PMOJA NA habari nyingine ikiwemo droo ya kombe la shirikisho Soma ..................................

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini anaamini kuwa kurejea kwa Jose Mourinho katika klabu ya  Chelsea kutaongeza uchangamfu wa ligi kuu ya soka nchini England Premier League na kuongeza kuwa kutaifanya klabu hiyo kuwa klabu ya tatu katika haraki za kuwani taji msimu ujao.
Baada ya kuwa katika msimu wa shida kwa meneja wa huyo mwenye umri wa miaka 50 sasa kuna tetesi za kutaka kurejea katika klabu yake hiyo hya zamani na kuihama Real Madrid huku tayari zikiwepo habari za chini chini kuwa tayari ameshakubaliana mambo ya msingi na klabu yake hiyo ya zamani baada ya miaka 6 kupita tangu aihame
Mancini amenukuliwa na Gazetta Extra Time akisema
"itakuwa ni uchangamfu mpya wa ligi na Chelsea itakuwa katika vita ya kuwania taji,"
Chuck Blazer apigwa stop kazi ya utendaji wa FIFA na CONCACAF
Baada ya kutuhumiwa kufanya makosa ya kimaadili ya utendaji ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, mtendaji mkuu wa shirikisho la soka la Marekani ya kaskazini, kati na Caribbean CONCACAF, Chuck Blazer ameadhibiwa.
FIFA imetangaza adhabu hiyo jana kwamba Blazer amefungiwa kwa kipindi cha siku 90.
Blzer mwenye umri wa miaka 68 ametuhumiwa kuchukua zaidi ya dolari za kimarekani milioni $20 kutoka CONCACAF wakati wa kipindi chake cha uongozi kama katibu mkuu.
Taarifa ya FIFA imesomeka kuwa
"mwenyekiti wa kitengo cha kisheria na maadili cha FIFA Hans-Joachim Eckert, ameamua kumfungia mjumbe wa kamati ya utendaji wa FIFA Chuck Blazer kutokushughulika na shughuli zozote za soka kuanzia ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa kipindi kisicho pungua siku 90.
"Mamuzi hayo yanafuatia ombi la kaimu mwenyekiti wa kitengo cha uchunguzi wa kimaadili Robert Torres, kutokana na kuonekana kwa uvunjifu mkubwa wa kimaadili uliofanywa na Chuck Blazer. "
Sunil Gulati ameteuliwa kushika nafasi ya Blazer katika kamati na ameahidi kuwa muwazi katika yote ya kibadhirifu yaliyotokea katika kipindi cha uongozi wa CONCACAF chini ya Jack Warner na Blazer.
Blazer anatarajiwa kujiuzulu mwenyewe kutoka katika uongozi wa FIFA May 30.
Balotelli kupigwa faini
 Mtendaji mkuu wa AC Milan Adriano Galliani amethibtisha kuwa Mario Balotelli atakumbana na adhabu baada ya kushangiliwa kwa kuvua jezi katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Torino ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia ambapo Balotelli alivua jezi yake baada ya kufunga goli pekee la ushindi.
Hata hivyo Galliani ameonyeshwa kufurahishwa na kasi ya ufungaji mabao ya Balotelli mwenye umri wa miaka 22 ambapo sasa ana magoli 9 kati ya michezo 10 ya Serie A aliyocheza.
Amenukuliwa akisema
"kwa kuwa anafunga magoli zaidi kuvua jezi hilo si tatizo lakini ieleweke kuwa kuvua jezi haikubaliki "
Tello: Sijafikia uwezo wa Henry bado.
 Cristian Tello amesema kuwa bado hajafikia uwezo wa Thierry Henri na kwamba bado ana safari ndefu ya kufikia na kulinganishwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona.
Tello mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akilinganishwa na nyota huyo mqwenye heshima kubwa na alama muhimu katika klabu ya Arsenal kufuatia aina yake ya ushambuliaji katika sehemu ya ushanbuliaji wa kushoto ya Blaugrana ambapo mwenyewe amekataa na kuweka wazi kuwa bado kufikia kiwango cha mfaransa huyo.
Amenukuliwa na Barca TV akisema
"bado nina safari ya kufikia soka na magoli yake "
Hata hivyo Tello alienda mbali zaidi na kuzungumzia umuhimu wa mshambuliaji Lionel Messi ndani ya Barcelona ambapo amesisistiza kuwa kukosekana kwake kulionyesha wazi umuhimu wake katika mchezo wa pili wa marudiano dhidi ya Bayern Munich katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Wapinzani wa soka la Moroccan wakutanishwa kombe la shirikisho hatu ya 16
 Timu mbili za Moroccan FUS Rabat na FAR Rabat zimekutanishwa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya shirikisho hatua ya 16 michezo ya play-off .
Timu hizo mbili ambazo zinatumia uwanja mmoja wa Prince Moulay Abdellah watakutana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi ikiwa ni michuano ya pili mikubwa ya ngazi ya vilabu barani Afrika.
Hatua hii ni ya michezo miwili ya nyumbani na ugenini ambapo timu 8 zilizoshindwa kutoka michuano ya klabu bingwa Afrika zinaunganishwa katika hatua 16 bora ya michuano yua shirikisho kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi.
Michezo ya kwanza itapigwa May 15 mpaka 17 huku michezo ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa May 31 na June 2.
Pamoja na mchezo huo wa timu ndugu toka Morocco pia TP Mazembe baada ya kushindwa na Orando pirates ya Afrika kusini sasa wamepngwa kucheza na Liga Muculmana ya Mozambique.
Muculmana ambao katika mchezo wa hatua ilipita waliwapeleka puta Wydad Casablanca ambao walipona kwa sheria ya faida ya bao la ugenini sasa wanakumbana na kigogo kingine Mazembe.
Wamisri wengine wa Enppi wamepangwa kukutana na St George ya Ethiopia ambao waliwapa shida Zamalek katika mchezo wa hatua iliyopita ya klabu bingwa Afrika.
CA Bizertin ya Tunisia iliyotolewa na mabingwa Al Ahly watakuwa na kazi kubwa kuwafungasha virago Ismaili ya Misri.
Washindi  8 wa michezo hiyo ya play-off  watatengeneza makundi mawili ya timu nne ambayo washindi wa kwanza na wa pili watasonga mbele kwa nusu fainali.
Droo hii hapa
Stade Malien (Mali) v Lydia LB Academic (Burundi)
Enugu Rangers (Nigeria) v CS Sfaxien (Tunisia)
FUS Rabat (Morocco) v FAR Rabat (Morocco)
CA Bizertin (Tunisia) v Ismaili (Egypt)
Entente Setif (Algeria) v US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia (Algeria) v Etoile du Sahel (Tunisia)
TP Mazembe (DR Congo) v Liga Maculmana (Mozambique)
St George (Ethiopia) v Enppi ( Egypt)
back to top