PICHA 5 ZA WANAFUNZI WA MANZESE WALIOVAMIWA NA MASHETANI LEO ASUBUHI
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini
Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku
wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu
kutanda maeneo hayo.
Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi
ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati
wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha
kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na
kupigana kama vichaa.