
Wanataaluma wengi wanapinga uamuzi
wa serikali kuyafuta matokeo ya kidato cha nne kwa madai
kwamba hilo siyo suluhisho la la tatizo ......

Wasomi hao wanadai kwamba hiyo ni
njia ya serikali kujisafisha kisiasa na kukwepa kujiuzulu kama
njia mojawapo ya kuwajibika....
Wakitoa maoni kwa nyakati tofauti, wanataaluma hao wanaamini kuwa, upungufu wa walimu, mgogoro ulipo baina ya serikali na walimu, nidhamu mbovu shuleni ( baada ya serikali kuzuia matumizi ya viboko), ukosefu wa vitabu na maktaba ndo vitu vya msingi ambavyo vimesababisha ubovu wa matokeo......
Miongoni mwa wanataaluma waliopaza sauti hadharani ni Makamu mkuu wa chuo cha Saint Augostine, SAUT....
Akiongea katika kipindi cha Tuongee asubuhi leo, Makamu mkuu wa chuo cha SAUT Father
Charles Kitima amesikika akilaani kitendo cha serikali kuyafuta matokeo ya kidato cha nne...
Kitima alisema wanaosema mitihani
isahihishwe upya hawana vision ya nchi hii kwani wako Bungeni kupiga
madawati na kufundisha watoto matusi na kwamba hawana weledi wa kuongoza
nchi hii.