MABINTI WATOANA MANUNDU WAKIGOMBEA MWANAUME
Warembo wawili, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam
ambao majina yao hayakupatikana, wamenaswa wakizichapa laivu wakidaiwa
kugombea bwana.
Tukio hilo la
kujidhalilisha lilijiri katika baa maarufu ya Corner iliyopo
Sinza-Afrikasana, Dar, majira ya asubuhi wakati watu wakiwa kwenye
mishemishe za kuwahi kazini.
Katika tukio hilo, mmoja wa warembo hao
alikuwa akilalamika kuwa kuna mwanaume walikubaliana kwenda kuvunja amri
ya sita fastafasta ili awahi kazini lakini akazidiwa ujanja na shosti
wake hivyo akataka kukomboa chake na ndipo alipotolewa manundu.
Habari
kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa warembo hao walijikuta wakizichapa
kavukavu wakimgombea mwanaume huyo aliyedaiwa kuwa ni mume wa mtu,
mwenye ndoa changa.Katika timbwili hilo lililojaza kadamnasi,
wanaume walishuhudia sinema ya bure baada ya mmoja wa warembo hao kula
kipigo kizito na kuvuliwa nguo ambapo alibaki wazi sehemu za makalio.