WASANII 5 WA MAIGIZO WALIOACHA KUIGIZA NA HIZI NDIYO KAZI WANAZOZIFANYA HIVI SASA.

Hawa jamaa walikuwa vizuri sana enzi hizo kwenye tasnia ya maigizo lakini leo hii hawapo tena kikamilifu kwenye tasnia ya maigizo, muda wao mwingi wanautumia kwenye kazi zao mpya. Kila mmoja hapa ameshawai kufikia pick na kufanya vizuri kwenye muda tofauti kwenye tasnia ya maigizo ndani ya michezo tofauti,Sasa cheki kazi wanazofanya sasa hivi.
SEKI
522529_494809150556310_558857778_n

Mmmoja kati ya watu ambao wamepitia sehemu nyingi na kufanya nazo vizuri sana ni jamaa Sekioni David “SekionDavid’sSon” kama alivyokuwa anajiita kwenye show yake ya City Sound. Seki alifanya vizuri sana kwenye maigizo na kundi la mambo hayo akiigiza role ya kijana mtukutu na mwizi ofcoz. Baadaye jamaa akageukia kwenye utangazaji kwenye show ya CitySound na baadaye CitySound2 ambazo zote mbili zilikuwa moja kati ya show bora sana za kila siku kwa kipindi kile au labda hadi leo bado hakuna show ya aina ile ilifikia that pick.Mara akaachana na huko na sasa anajihusisha zaidi na kundi la Ze comedy ambapo yeye ndiyo producer nyuma ya pazia . Kama unaona mzunguko wa Seki alikuwa kwenye tasnia ya maigizo,akaingia utangazaji na baadae amerudi tena lakini akiwa kama muandaaji na sio muigizaji. All in all tunaamini Seki anaweza kufanya vizuri tena akirudi kufanya kazi za uigizaji tena, especially kwenye serious movies ambazo ndiyo zinafanya vizuri sokoni.
KIPEMBA
IssaKipemba1
Kipemba habari zilizopo ni kwamba kaka mkubwa siku hizi ni mtumishi wa umma kwa kupitia jeshi la polisi kwa maana ya kwamba amekuwa polisi. Kuna movie moja ambayo amefanya Kipemba na Jacklyne Wolper wakiwa kama maaskari wapelelezi, so kwenye hiyo movie ni kwamba ame-act uhalisia wa kazi yake ya sasa. Kipemba kama unakumbuka alikuwa ni mmoja kati ya waigizaji wakali ndani ya Kaole Sanaa Group.
SIMALENGA
Simalenga Simon
Public Relation manager wa Clouds Media Group kwa sasa na mmoja kati ya waigizaji wa Kaole Sanaa Group japo zamani. Kaka huyu ambaye kwa taaluma yake ni uandishi wa habari na amewahi kifanya kazi na show kama Jahazi na Njia Panda zote za Clouds FM, ameipotezea kabisa tasnia ya uigizaji na sasa yupo busy mjengoni.
All is well kwake kwasababu amefikia pazuri kwa kupata position kubwa kwenye media house kubwa kama Clouds Media Group.

ZEMBWELA
5SELEKT 016
Kipindi hicho alikuwa anakamata macho mengi akiwa na mshkaji wake marehemu Max kwenye comedy ya Max na Zembwela. Lakini siku hizi anakamata maskio ya watu kupitia airwaves za EastAfrica radio kwenye show ya SuperMix. Zembwela ana-run show ambayo inasikilizwa sana kwa mida ile na inahusisha sana contenct za kisiasa na kijamii bila kusahau burudani. The good thing ni kwamba jamaa bado hajaacha kipaji chake kwasababu mara nyingi anaendesha show yake katika mfumo wa comedy lakini muda huo huo akifikisha ujumbe alioukusudia.
Kama sasa hivi Zembwela ameongeza umaarufu wake kupitia radio show inaweza kuwa ni njia nzuri au wakati mzuri wa kurudi kwenye kazi yake ya zamani na pia kuendelea na kazi yake ya sasa.
BI HINDU
dida3
Mama huyu anamaneno mia kadhaa ndania ya dakika moja, akiongea huwezi lazima upige kimya kwa maneno mengi na mazito ya kushushua atakayokupa. Bi Hindu siku hizi nayeye hayupo sana kwenye maigizo na badala yake unaweza kumsikia kwenye radio show za Times FM akifanya segment kadhaa kwenye show ya taarab.
Bi mkubwa kutokana na maneno yake mengi ya mipasho ame-fit vizuri kwenye show hiyo ambayo inaongozwa na  Dida wa Mchops alafu wote wawili wana wingi wa maneno.
back to top