
Msanii
anayetafuta mafanikio kwa kasi, Wema Sepetu amesema kuwa haoni sababu
ya watu kutishiana maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yapo
juu.
Wema
alisema hayo kufuatia hivi karibuni kutishiwa maisha na watu
asiowafahamu na kulazimika kuongeza ulinzi nyumbani kwake na kila
anapokuwa anatoka.
Alisema
maisha ni magumu na kila mmoja anatakiwa afanye kazi kwa bidii ili
kufikia malengo, badala yake watu wanaanza kutishiana maisha.
"Nawashangaa
watu wanaoendelea kuwafuatafuata wengine wanapata wapi ujasiri huo na
hali ya maisha ilivyo ngumu na kuhitaji muda mwingi wa kufanya kazi
ili kujikwamua,"alishangaa Wema.
Aidha,
aliongeza kuwa hana adui wala mtu ambaye anamdai au kitu kama hicho
hivyo watu wanaomtumia mesaji za vitisho anahisi wana chuki binafsi
na si kingine.