
Wakati
kambi ya timu ya taifa ikiingia siku yake ya pili hii leo kwa ajili ya
maandalizi ya michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa, taarifa zinasema
ni wachezaji 6 tu ndio walioripoti kambini mpaka kufikia jioni ya leo.
Akiongea
na Rockersports kocha msaidizi wa timu hiyi Sylvester Mashi amesema
hali hiyo imetokana na wachezaji wengi kuendelea kuwepo katika timu zao
ambazo zimekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Yanga yenye
wachezaji 5 wa timu ya taifa ambao bado wako nchini Uturuki wakiendelea
na kambi ya wiki mbili.
Kwa
upande wa wachezaji wa Simba wao bado wanaendelea na michuano ya kombe
la Mapinduzi visiwani Zanzibar ambapo Mashi amesema wanategemea kuwapata
wachezaji hao usiku wa leo na kufanya idadi ya wachezaji 12 idadi
ambayo itawawezesha kuanza mazoezi hapo kesho.
Kwa
upande wa wachezaji wa Azam fc Mashi amesema wanategemea kuwapata hapo
kesho kwani wanasubiri mchezo wao wa leo wa michuano ya kombe la
Mapinduzi.
Kuhusu
wachezaji wa Yanga Mashi amesema shirikisho la soka nchini TFF
linaendelea na mchakato wa kuwapata wachezaji hao mapema na kwamba
wanaimani kuwa wachezaji wa timu ya taifa walioko katika kambi ya Yanga
watawahi safari ya Afrika kusini.
Taifa
stars inawachezaji 5 kutoka Yanga ambao ni Kelvin Yondan, Frank Domayo,
Athumani Iddi Chuji, Simon Msuva na Nadir Haroub Kanavaro.
Kutoka Simba ni Amir Maftaha, Mwinyi Kazimoto, Juma Kaseja, Shomari Kapombe na Amri Kiemba.
Kutoka Azam fc ni Erasto Nyoni, Salum Abubakar, Khamis Mcha, Aggrey Moris, Aishi Manula na John Bocco.
Wachezaji
ambao wamesha ripoti kambini ni pamoja na Juma Kaseja , Issa Rashid,
Aggrey Morris, Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa.
Taifa
Stars inataraji kuelekea nchini Ethiopia kwa mchezo wa kimataifa wa
kirafiki tarehe 11/01/2013 dhidi ya wawakilishi hao wa kanda ya Afrika
mashariki na kati katika fainali za mataifa ya Afrika.
Kwa
vyovyote vile inaonekana kuna uwezekano mdogo wa kambi hiyo ya timu ya
Taifa kuwapata wachezaji wa Yanga ambao programu yao mazoezi ya wiki
mbili itakamilika mwishoni mwa juma hili.
Kwa
upande wa Simba nao wanajipanga kwa safari ya kuelekea nchini Oman kwa
kambi ya maandalizi ya ligi kama ilivyo kwa Yanga ambao wanaendelea na
kambi hiyo nchini Uturuki ambapo bila shaka watahitaji kuelekea huko na
wachezaji wao wote.
Aidha
kwa upande wa Azam yenye dhamira ya kutetea taji lao la kombe la
mapinduzi hivi sasa wanaendelea vema na michuano hiyo ambapo nao
watataka kuendelea kuwatumia wachezaji wao mpaka fainali endapo watapata
nafasi ya kufika katika hatua hiyo ya michuano hiyo.
Hata
hivyo kocha msaidizi Mashi anaamini kwa jitihada za TFF watafanikiwa
kuwapata wachezaji wote waliotajwa na kocha mkuu wa timu ya taifa Kim
Poulsen na kufanikisha programu ya timu ya Taifa ikiwa ni pamoja na
kufanikisha safari hiyo ya nchini Ethiopia.