Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Aden Rage ametoa mpya kwa
kusema kuwa hatambui chochote kuhusiana na mkataba ulioingiwa baina ya
timu yake na kocha wao mpya kutoka Ufaransa, Patrick Liewig.
Simba waliripotiwa kusaini mkataba wa miezi nane na Liewig ambaye amechukua nafasi ya kocha aliyewapa ubingwa katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mserbia Milovan Cirkovic.
Wakati wakisaini mkataba huo, Simba ambao awali walitangaza kuwa watamsainisha kocha huyo mkataba wa mwaka mmoja na nusu, waliwakilishwa na makamu mwenyekiti wao, Godfrey Nyange ‘Kaburu’.
Hata hivyo, alipoulizwa na NIPASHE jana kuhusiana na sababu za kumpa kocha Liewig mkataba ‘kiduchu’ wa miezi nane badala ya miezi 18 waliyotangaza awali, Rage ndipo alipotoa mpya kwa kusema kuwa yeye hajui chochote kuhusiana na mkataba wa kocha huyo.
Akieleza zaidi, Rage alisema kuwa hivi sasa yuko mapumzikoni mkoani kwao Tabora na ndiyo maana hajui makubaliano ya mkataba wao wa kocha huyo aliyewahi kuzifundisha klabu kadhaa kubwa barani zikiwamo za Asec Mimosas ya Ivory Coast na Club Africaine ya Tunisia.
“Mimi kwa sasa niko Tabora kwa mapumziko ya sikukuuu. Jukumu la mkataba wa kocha (Liewig) nililiacha kwa Makamu Mwenyeki (Kaburu),” alisema Rage.
“Kwa mujibu wa katiba ya Simba, mwenyekiti anapokuwa nje ya ofisi, makamu mwenyekiti anachukua nafasi ya mwenyekiti katika kuongoza klabu. Kwa hiyo muulizeni makamu (Kaburu) juu ya hilo,” alisema Rage.
Kaburu alipotafutwa hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo huku katibu mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala akikataa kuzungumza chochote kwa madai kwamba alikuwa na kazi nyingi.
“Kwa sasa nina kazi nyingi zimenibana, naomba unitafute baadaye,” alisema Mtawala.
Hata hivyo, alipotafutwa tena na gazeti hili jana saa 9:52 alasiri, hakupokea simu. Na hata zoezi hilo liliporudiwa saa 12:21, bado katibu huyo ambaye ndiye aliyetangaza awali kuwa watampa Liewig mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hakupokea simu.
Liewig alitua nchini Jumatatu na kupokewa kwa mbwembwe kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na viongozi na mashabiki wa Simba walioongozwa na Mtawala.