PICHA ZA LULU MICHAEL AKIWA HURU URAIANI.....
Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa
Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni
wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
--------------------------------
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es
Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael
'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu
Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha
taratibu zote za dhamana.