
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu, David Mziray
Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Herembe kilichoko Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Habari zilizopatikana kutoka kwa wanavijiji walioko eneo la tukio
zilieleza kuwa abiria zaidi ya 60 waliokolewa wakati wengine zaidi ya 25
hawajulikani walipo na 12 wakihofiwa kufa maji.
Kufuatia tukio wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Kigoma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali mstaafu Issa
Machibya wamekwenda kwenye eneo la ajali hiyo.
Hata hivyo kutokana na kukosa mawasiliano na pia Herembe kukabiliwa
na changamoto za kimiundo mbinu ilishindikana kupata taarifa za safari
ya boti hiyo iwapo ilikuwa ni ya ndani ama ilikuwa inafanya safari ya
nchi jirani.
Baadhi ya wanavijiji walidai kuwa boti hiyo ilikuwa inasafiri kati
kijiji cha mwambao cha Kalya kwenda bandari ya Kigoma wakati wengine
walidai ilikuwa njiani kuelekea Burundi.
Mashuhuda walisema boti hiyo ilikuwa na shehena ya dagaa na abiria
zaidi ya 100 na ilipinduka kufuatia dhoruba iliyosababisha kuyumba na
kugonga mwamba ,
Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma kupitia simu yake ya mkononi hazikufanikiwa.
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi
kavu (Sumatra), David Mziray alisema mamlaka hiyo ilikuwa haijapata
taarifa kuhusiana na kuzama kwa boti hiyo.
Aliahidi kufuatilia kupitia kikosi cha uokoaji ili kubainisha kile kilichojiri